NA TIMA SALEHE

UONGOZI wa Simba umesema kuwa wapinzani wao FC Platinum itakuwa ngumu kutoka kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Januari 6, uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salam

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ina kibarua cha kupindua matokeoa ya bao 1 – 0 ililofungwa kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa mjini Harare Zimbabwe.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameliambia gazeti hili kwamba wanatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila kwa namna yoyote ile itakuwa ngumu kwa wapinzani wao kutoka.

“Mashabiki wetu ambao ni mastaa namba moja ndani ya timu yetu tunawaomba wajitokeze kuipa sapoti timu yetu kwa kuwa hakuna namna mpinzani wetu hatoki pale kwa Mkapa.

Akizungumzia maandalizi na mipango kuhusu mchezo huo, manara alisema ipo vizuri na wanasubiri muda ufike ili tutoa burudani kwa mashabiki.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 inakibarua cha kusaka ushindi wa mabao zaidi ya mawili ili kusonga mbele.

Wapinzani wa Simba, FC Platinum tayari wapo nchini baada ya kuingia Disemba 2 mwaka huu ambapo wameweka wazi kwamba wamekuja kusaka ushindi.