NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa yaTanzania, Etienne Ndairagije, amempa pole mchezaji wake Bakari Mwamnyeto kwa kufiwa na mke na mtoto wake.

Mwamnyeto ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kambi ya timu ya taifa yaTanzania kujiandaa na mchezo wa kirafiki na michuano ya CHAN.

Timu ya Taifa inatarajia kuvaana na DRC Congo kesho kwenye Uwanja wa Mkapa na kurudiana Januari 13 nchini Congo.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana kwa njia y asimu Ndayiragije alisema amezipokea kwa masikitiko taarifa za msiba uliomkuta mchezajiwake .

Alisema  mchezaji huyo anatarajia kurudi kambini mapema mara baada ya kumaliza maziko hivyo nafasi yake ipo pale hatoita  mchezaji mwingine.