NA ABOUD MAHMOUD

MICHUANO ya kuwania kombe la Mapinduzi kwa mchezo wa mpira wa wa mikono (Handball) imeendelea katika viwanja vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Migombani kwa kuzikutanisha timu mbali mbali.

Katika mashindano hayo KMKM wanawake walishindwa kutamba baada ya kufungwa mabao  28 – 23 na mabati wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Nayo timu Victory wanawake ilifanikiwa kuondoka na ushindi baada ya kuwatandika Wete mabao 12 – 6.

Aidha kwa upande wa wanaume timu ya Wete kutoka kisiwani Pemba ilifanikiwa kuondoka uwanjani hapo ikiwa na furaha baada ya kuwafunga Miwani mabao 11 – 5.

Katika hatua nyengine michuano hiyo zikutanisha timu za vijana ambapo wanaume Miwani ikaondoka na ushindi wa maabo 26 -6 dhidi ya Mlamleni.

Nao Wete waliondoka uwanjani hapo wakiwa washindi wa mamabao 22 -7 dhidi ya  Mlaleni , huku Victory ilijinyakulia ushindi wa mabao  31- 7 dhidi ya Miwani.

Kwa upande wa wanawake vijana  Victory waliondoka na  ushindi kwa kuwafunga Miwani mabao 13 -8.