WATU wengi hufikiria kwamba kukokwa na mikojo kitandani mara nynegine ni kitu kinachowatokea watoto pekee, lakini ni tatizo ambalo pia linaweza kuwakumba watu wazima.

Unaweza kuamka na kuhisi aibu baada ya kujikuta umetokwa na mikojo kitandani, lakini sio makosa yako.

Inawezekana kwamba hilo limefanyika kutokana na tatizo la kiafya, dawa unazotumia, ama tatizo la kibofu chako cha mkojo.

Hatahivyo kuna njia nyingi za kutatua. Utafiti unaonesha kwamba asilimia mbili ya watu wazima wana tatizo la kutokwa na mikojo kitandani.

Daktari Salihu Kwaifa, mtaalamu katika hopsitali ya Wuse mjini Abuja alisema kwamba kwa watoto kati ya umri wa miaka mitano hadi kumi sio ugonjwa bali ishara za kukua.

Hata hivyo, kwa mtu mzima kuanzia umri wa miaka 18 anapokojoa hudaiwa kuwa ugonjwa.

Tovuti ya Health website WebMd inaelezea baadhi ya matatizo ya kiafya yanayosababisha hali hiyo miongoni mwa watu wazima ambayo hushirikisha matatizo ya kibofu cha mkojo, kuwa na wasiwasi ama matumizi ya dawa nyengine.

Sababu zinazowafanya watu wazima kutokwa na mikojo kitandani

Figo zako huenda zinatengeneza mikojo mingi zaidi ya kiwango kinachohitajika.

Homoni kwa jimna ADH huambia figo zako kutengeneza mkojo michache ya kiwango cha kawaida na mara nyingi homoni hiyo hupungua nyakati za usiku.

Wakati unapotokwa na mikojo kitandani huenda homoni za ADH zimepungua ama figo zako hazifanyi kazi kama inavyohistahili.

Kisukari kwa jina diabetes insipidus pia huathiri kiwango cha homoni cha ADH, hatua inayozifanya figo zako kutengeneza kiwango cha juu cha mikojo.

Kunapokuwa na mikojo mingi, kibofu chako hushindwa kuizuia na hivyobasi mikojo hutoka.

Wakati huohuo misuli ya kibofu chako cha mkojo hufunga wakati uko tayari kukojoa.

Lakini iwapo misuli ya kibofu cha mikojo hufunga na kufungua wakati usiohitajika, mwisho wake ni mtu kutokwa na mikojo.

Daktari Salihu anasema kwamba vidudu vya zamani ama kemikali zinazosababisha ongezeko la mikojo zinaweza kumfanya mtu kukojoa kitandani.

Mwanamke anaweza kuwa na tatizo la kukojoa kitandani iwapo ana tatizo la kibofu cha mkojo na anashindwa kuzuia mikojo.

Pia kuna maambukizi ya njia ya mkojo ambayo yanaweza kumfanya mtu mzima kukojoa kitandani.

Anasema kwamba watu wazima pia hupatikakana na tatizo hilo iwapo wamekumbwa na kiharusi ama tatizo la kiakili.

Daktari huyo pia ameongezea kwamba kuna dawa ambazo pia zinaweza kumfanya mtu kuwa na tatizo hilo.

Kwa wanawake ambao wamepata tatizo la kuavya mimba wanaweza kuwa na shida ya kwenda haja ndogo.

Pia kwa wale wanaokunywa maji mengi nyakati za usiku wakati wanapokwenda kulala ama wanapoamka wanaweza kutokwa na mikojo kitandani.

Kitamaduni tatizo la kutokwa na mikojo kitandani hudaiwa kusababishwa na pepo wabaya au mashetani.

Lakini daktari Salihu anasema kwamba kutokwa na mikojo ni ugonjwa ambao unapojulikana hauwezi kushirikishwa na pepo au mashetani.

Kwa wale wanaotumia dawa ambazo huwasababisha kukojoa mara kwa mara wanaweza kuwacha kutumia dawa hizo.

Vilevile kuna dawa ambazo hutolewa na daktari kuzuia kukojoa mara kwa mara.

Kwa wale wanaotokwa na mikojo wanapolala wanaweza kutokunywa maji mengi wakati wanapokwenda kulala.Vilevile mtu anaweza kuweka muda wa kuamka kwa kutumia saa ili aweze kwenda haja ndogo.