MUNICH, Ujerumani
MSHAMBULIAJI, Robert Lewandowski, amezungumza kwa maneno mazuri juu ya uhusiano wake na Jurgen Klopp, akisema, bosi huyo wa sasa wa Liverpool alikuwa ‘mwalimu mbaya’ ambaye alimchochea kwenye njia ya ukuu.

Baada ya kupata maisha magumu katika miaka yake ya ujana, Lewandowski alianza kufunga bao mara kwa mara akiwa Znicz Pruszkow na Lech Poznan, ambayo yalimfanya ahamie Borussia Dortmund mnamo 2010.

Kuanza kwa maisha kwa Lewandowski katika Bundesliga hayakuwa laini, kwani alicheza katika nafasi isiyoimudu ya nambari 10 na alipata maisha magumu kwenye mazoezi chini ya Klopp.

Mambo yalifikia hatua kufuatia kichapo cha Ligi ya Mabingwa dhidi ya Marseille mnamo Septemba 2011.
Lewandowski alimkabili Klopp na kumuuliza meneja wake ni nini anataka kutoka kwake.

Licha ya Mjerumani huyo kuwa mkali katika hatua hiyo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland alichukua kile kinachotakiwa kwake na mambo yalichanua kiasi kwamba alishinda taji la pili la Bundesliga kabla ya kupata uhamisho wa Bayern Munich.

Akifafanua jinsi uhusiano wake na Klopp ulivyokua kwa kukua wachezaji,Lewandowski alisema: “Jurgen hakuwa mtu wa baba tu kwangu. Kama meneja, alikuwa kama mwalimu ‘mbaya’. Na ninamaanisha kwamba kwa maana bora ya neno.