NA MWAJUMA JUMA

MZUNGURUKO wa tisa wa ligi kuu ya Zanzibar unatarajiwa kuanza kesho.

Ligi hiyo ambayo ilisimama kupisha michuano ya kombe la mapinduzi ya mpira wa miguu, inatarajiwa kuchezwa mechi tatu katika viwanja vitatu tofauti.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na bodi ya ligi inaonesha katika kisiwa cha Unguja kutakuwa na mechi mbili na moja itachezwa katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.

Ratiba hiyo inaonesha Malindi itaanza mzunguruko huo kisiwani Pemba kwa kucheza na Hard Rock.

Malindi inashuka dimbani hapo ikiwa na majeraha ya kufungwa mechi mbili mfululizo.

Michezo mengine miwili ya mzunguruko huo ni Black Sailor itaumana na JKU mchezo ambao utachezwa uwanja wa Mao Zedong A na katika uwanja wa Amaan Kipanga itacheza na Chuoni.

Wakati ligi hiyo inaendelea mzunguruko wa tisa hadi sasa jumla ya mabao 94 yamefungwa  michezo 44 iliyochezwa.

Ligi hiyo inashirikisha timu 12 zikiwemo Mlandege, Polisi, KMKM, Malindi, Kipanga, Hard Rock, Chuoni, Zimamoto na Mafunzo.