ZASPOTI
KOCHA Mkuu wa Uganda, Johnathan McKinstry, amesema, Halid Lwaliwa ameteuliwa kuwa nahodha wa timu hiyo kwa sababu alikuwa ameongoza vizuri kwenye michuano ya Kombe la Chalenji Afrika Mashariki na Kati.


Beki huyo atakuwa akiongoza nchi yake kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Chan) akitarajia kuisaidia Cranes kufanya vizuri. Bosi huyo wa ufundi kutoka Ireland Kaskazini pia alisema mchezaji huyo wa Vipers SC atasaidiwa na wachezaji wengine wakubwa.


“Kama nahodha wetu, alikuwa akihudumu vizuri zaidi ya mwaka jana, pamoja na kuvunja timu ya wakubwa ya Cranes,” McKinstry alielezea.
“Atasaidiwa na kundi la wachezaji wakubwa wanne au watano ambao watatakiwa kuchukua kitambaa cha unahodha kufanya kazi pamoja na Halid ili kutoa hali nzuri.”


Cranes walishiriki katika mashindano ya kabla ya Chan yaliyofanyika nchini Cameroun katika wiki ya kwanza ya Januari. Walitoka sare ya bao 1-1 na Indomitable Lions kabla ya kuifunga Chipolopolo 2-0. Siku ya Alhamisi, walifanikiwa kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Niger na kumaliza mashindano hayo kwa kiwango cha juu.


Kocha huyo mchanga ameelezea ni kwanini mashindano hayo yalikuwa muhimu kwake na kwa timu kwa ujumla.
“Kambi hii imekuwa sio ya thamani kubwa kwetu tu bali pia ni changamoto kubwa kwetu kama timu ya makocha katika kuchagua kikosi cha mwisho”, McKinstry, aliendelea.


“Ikiwa ni muaminifu, tulitumia zaidi ya masaa matatu kuchagua timu ya mwisho. Tulitaka kuhakikisha kuwa kila mchezaji anapata nafasi nzuri, sio tu kwa kucheza na wakati wa mazoezi kwenye mashindano haya madogo, lakini, pia katika kujadili faida na hasara za kila mchezaji.
“Wakati wa kuchagua timu ya mwisho, tulitaka usawa kwenye kikosi. Tulihitaji mpango ‘B’ kulingana na wapinzani, lakini, pia tukazingatia utendaji wa kila mtu.”


Cranes wapo katika kundi ‘C’ na mabingwa watetezi Morocco, Rwanda na Togo.
Kikosi kamili kinaundwa na walinda milango, Lukwago Charles (KCCA FC, 1), Mutakubwa Joel (Kyetume FC), Alionzi Legason Nafian (URA FC) na Ikara Tom (Police FC).
Walinzi ni Hassan Muhamud (Police FC), Kayondo Abdu Aziizi (Vipers SC), Mujuzi Mustafa (Kyetume FC), Ssenjobe Eric (Police FC), Iguma Denis (KCCA FC), Willa Paul (Vipers SC), Lwaliwa Halid (Vipers SC) na Mbowa Paul Patrick (URA FC).


Viungo ni pamoja na Mawejje Tonny (Police FC), Kagimu Shafik Kuchi (URA FC), Anukani Bright (KCCA FC), Kyeyune Saidi (URA FC), Byaruhanga Bobosi (Vipers SC) na Watambala Abdu Karim (Vipers SC).
Washambuliaji ni Ojera Joackim (URA FC), Brian Aheebwa (KCCA FC), Ocen Ben (Police FC), Viane Ssekajugo (Wakiso Giants FC), Orit Ibrahim (Vipers SC), Muhammad Shaban (Vipers SC) na Karisa Milton (Vipers SC). (Goal).