NA VICTORIA GODFREY

CHAMA cha Judo Zanzibar ( ZJA) kimeanza maandalizi ya mashindano ya ubingwa wa Afrika Mashariki ambayo yamepangwa kufanyika Machi 4 hadi 8 mwaka huu Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa ZJA, Mohamed Khamis Juma, alisema maandalizi yanakwenda vizuri.

Alisema mialiko imetokea kwa vyama na mashirikisho ya mchezo huo Afrika Mashariki ili kuandaa timu zao na kujiweka tayari kwa mashindano hayo.

“Maandalizi yanaendelea kufanyika ili kuhakikisha yanafanyika kwa uweledi na ushindani mkubwa kwani tunaamini timu zitakuwa zinajiandaa kikamilifu,” alisema Juma.