NEW DELHI, INDIA

MAHAKAMA ya juu ya India imesitisha kwa muda utekelezaji wa sheria za mageuzi ya kilimo na kuamuru uundwaji wa kamati huru ya wataalamu watakaofanya majadiliano na wakulima, wanaopinga sheria hizo.

Uamuzi huo wa mahakama umekuja siku moja baada ya kusikilizwa kwa mashauri yaliyowasilishwa na wakulima yakipinga sheria hizo.

Katika uamuzi wake mahakama ilisema sheria hizo zilipitishwa bila ya kufuata ushauri wa kutosha na inakatisha tamaa kwa namna mazungumzo yanavyoendelea baina ya wawakilishi wa serikali na wakulima.

Maelfu ya wakulima wanaopinga sheria hizo wamekuwa wakizuia barabara kuu nje ya mji mkuu wa New Delhi kwa zaidi ya siku 45.