LONDON, England
MANCHESTER United ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji wa AS Roma, Edin Dzeko.

Dzeko alipelekwa kwa mkopo Roma msimu wa 2015/16 akitokea Manchester City ambapo akiwa Etihad alicheza mechi 130 na kufunga magoli 50.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 awali iliripotiwa kuwa, Pep Guardiola anamuhitaji kabla ya kupotezea dili hilo jambo linalowapa nafasi United kuipata saini yake ili awe mbadala wa Odion Ighalo ambaye amerudi Shangai Shenhua ya China.
Dzeko inaelezwa kuwa hayupo kwenye uhusiano mzuri na kocha mkuu wa Roma, Paulo Fonseca jambo linalomfanya afikirie kuondoka.(Goal).