KUNA vivutio vingi vya utalii duniani ambayo huwafanya watu kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine kwenda kuvishuhudia kwa kufanya utalii.

Moja kati ya vivutio vikubwa duniani vya utalii ni maporoko ya maji ambapo aghabu huwa mto unaotiririsha maji unapokutana na sehemu ya bonde lililokatika katika sehemu hutokea maporomoko ya maji.

Maeneo mengi duniani yana maporomoko ya maji, hata hivyo katika makala haya nataka nikuonesha baadhi ya maeneo ya maporomo ya maji yanayovutia zaidi duniani.

Maporomoko ya Rhine, Uswisi

Maporomoko ya Rhine huko Schaffhausen, ambayo yapo kilomita chache kutoka ziwa Constance, yana urefu wa mita 23 na upana wa mita 150. Wageni wengi wanaofanya utalii katika eneo hilo wanaweza kuona uzuri wa asili ya eneo hilo kutoka maeneo kadhaa.

Sehemu nyingine ya kuvutia katika eneo la maporomoko hayo ni uwepo wa kasri dogo la Wörth, ambalo liko kwenye kisiwa, maji yanayoporomoka katika eneo hilo yanaweza kuonekana kwa uzuri zaidi moja kwa moja kutoka kwenye boti.

Maporomoko ya Viktoria, Zambia/Zimbabwe

Maporomoko ya Victoria ni miongoni mwa turathi ya dunia na yapo katika nchi mbili za Afrika ambazo ni Zambia na Zimbabwe.

Maporomoko ya Victoria yana upana wa mita 1708 ambazo ni sawa na futi 5604 na yanachukuliwa kuwa maporomoko ya maji mapana zaidi ulimwenguni.

Maporomoko hayo yana hadi mita za ujazo 10,000 za maji, lakini mto Zambezi hauna uwezo wa kuchukua maji mengi kila wakati kiasi kwamba katika msimu wa ukame maji hupungua sana.

Maporomoko ya Niagara, USA/Canada

Maporomoko ya Niagara yaliyoko mpakani baina ya Marekani na Canada. Maporomoko hayo yamepewa jina la India la “maji yanayounguruma” kulingana na msimu.

Yana mita za ujazo 2,800 hadi 5,700 kwa sekunde (98,881 hadi mita za ujazo 201,293 kwa sekunde) na kumwagika kwenye vilindi hivi. Maporomoko ya Niagara yana milango mitatu ya maji ambayo ni maporomoko ya Marekani, Maporomoko ya Bridal Veil na maporomoko ya Horseshoe.

Maporomoko ya Iguazú, Brazil/Argentina

Maporomoko mengine ya maji ni ya Iguazú ambayo yanapatikana mpakani baina ya mataifa mawili ya Brazil na Argentina.

Hapa, maporomoko 275 huingia ndani ya bwawa lenye urefu wa mita 700 na upana wa mita 150 ni miongoni mwa kivutio hiki cha asili pia kimetangazwa kuwa turathi ya dunia.

Maporomoko ya Ban Gioc Detian, China/Vietnam

Maporomoko ya Ban Gioc Detian yako kwenye mpaka kati ya China na Vietnam.  Mto Quy Xuân humwaga maji katika eneo la upana wa mita 300 wa ukuta wa mwamba wa zaidi ya mita 50.

Mto huo huchukua kiwango kikubwa cha maji kati ya mwezi wa Mei na Septemba. Jambo la kipekee juu yake ni kwamba mazingira yake ni kama ndoto. Ukiangalia maji yanavyoporomoka utahisi kama filamu ya kufikirika.

Maporomoko ya Angel Falls, Venezuela

Ni maporomoko ya kina kirefu zaidi duniani yapo mita 979 ambazo ni sawa na futi 3,211 ft) kutoka kilele cha mlima Auyan-Tepui huko Venezuela. Yanatokana na Mto wa Río Churún.

Yanapomwagika chini, maji huonekana kama matone madogo ambayo hugeuka kuwa mto unaoenda kwa kasi. Salto Ángel, kwa Kispaniola, ni sawa na Maporomoko ya Malaika. Sio rahisi kuyafikia – hufikika tu kwa ndege ama safari ya siku moja ya boti.

Maporomoko ya Gullfoss, Iceland

Iceland hutambulika kama kama kisiwa cha moto na barafu. Ni mahali ambapo kuna barafu na kuna maji mengi. Vivyo hivyo kwa mto mkubwa kabisa Gullfoss (Maporomoko ya Dhahabu).

Una upana wa mita 229. Yako katika njia kunakopatikana vivutio vya maduara ya dhahabu na yanafikika kirahisi. Ni njia inayoongoza kwenye eneo ambalo watalii wanaweza kuyafurahia maporomoko ya maji kwa karibu.

Maporomoko ya Seljalandsfoss, Iceland

Iceland ina maelfu ya maporomoko ya maji. Lakini Seljalandsfoss yaliyoko kusini mwa kisiwa hicho ndio maarufu zaidi. Hapa wageni wanaweza maporomoko wakiwa nyuma ya maji, lakini pia mazingira yake. Na hususan nyakati za jioni, rangi huonekana kali sana. Hufaa sana kwa picha. Maporomoko hayo ya maji yana urefu wa mita 66 na maji yake hutokea Mto wa Seljalandsá.

Maporomoko ya Ouzoud, Morocco

Maporomoko ya Ouzoud kwenye ukingo wa Milima ya Atlas ndio milango ya maji ya juu zaidi na yenye maji mengi huko Moroko. Maporomoko ya maji madogo madogo humwagika mita 110 juu ya miamba yenye rangi nyekundu na mwishowe hutiririka ndani ya ziwa dogo. Wageni wanaweza kushuka kutoka juu kupitia njia ya miguu.

Hifadhi ya taifa ya maziwa Plitvice, Croatia

Maziwa ya Plitvice pia ni sehemu ya turathi ya Ulimwengu iliyotajwa na UNESCO na ni ukumbusho wa watalii wa Croatia. Maporomoko hayo yanaunganisha maziwa 16 yaliyopangwa kwa hatua.

Hifadhi hiyo ya kitaifa iliyo na maziwa na maporomoko ya maji mengi inaweza pia kutembelewa kupitia barabara zinazokwenda mlimani, kwa boti au kwa treni ya watalii.