NA LIGWA PAULIN
MASHEHA wa jimbo la Fuoni Wilaya ya Magharibi “B”, wameamua kupita kila mtaa kukusanya maoni yatayoimarisha utoaji huduma bora, ikiwemo ya utunzaji wa mazingira na kupiga vitendo vya udhalilishaji.
Hatua hiyo inakuja ikiwa sehemu ya kuukaribisha mwaka mpya 2021, ambapo Sheha wa Sheia ya Kipungani, Maritina Raphael Daneil, alisema wameamua kuchukua hatua hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la seriali ya awamu ya nane linalowataka kuwa karibu na wananchi.
Alisema Masheha wamepwa agizo la kufika kila mtaa na kila nyumba kutokana na matatizo yanayojitokeza katika jamii, lengo likiwa ni la kueleimsha, kuonya pamoja na kupata maoni tofauti hasa yanayohusiana na watu wanaofanya maovu mbalimbali katika maeneo yao na kuchukua hatua.
Maritina ambae pia anakaimu nafasi ya Sheha wa Fuoni Migombani ambaye yuko likizo alisisitiza kuwa watu wanaotiririsha maji machafu na kutupa taka ovyo wakibainika atawachukulia hatua hapohapo.
“Hakuna kuoneana haya sasa kama una mtu mwizi, kibaka, mdhalilishaji , anayehatarisha usalama kwa namna yeyote ile katika mtaa wenu au nyumba jirani semeni sasa “. Alisitiza kwa ukali Sheha huyo.
Akijibu hoja alisema wale wanaohitaji vyeti vya kuzaliwa waende ofisini kwake au maeneo walikozaliwa watapewa utaratibu na wasipata vyandarua waende kwa mabalozi wao.
Akikagua baadhi ya nyumba zinazotiririsha maji na kuwataka wenye moboma ya nyumba yalio wazi wayafanyie usafi pamoja na kuweka milango, ili kuzuia vitendo viovu na kutupa taka.