NA ZAINAB ATUPAE

MASHEHA wa jimbo la Malindi wamegizwa kufanya vikao vya mara kwa mara na wananchi wao, ili  wananchi  kupata nafasi ya kutoa changamoto zao na baadae kuwapelekea  viongozi wao wa jimbo.

Agizo hilo limetolewa na Uongozi wa jimbo hilo katika skuli ya Tumekuja wakati walipokuwa wakizungumza na wanachi wa shehiya ya Mkunazini na Shangani  katika hatua za mwisho za kusikiliza changamoto za wananchi wao.

 “Lengo la serikali kutatua changamoto za wananchi, hivyo nivyema kufanya hivyo mara kwa mara, ili kutambua na zipi zilizofanyiwa kazi,”alisema.

Suleiman Mohamed Mbunge wa jimbo hilo na Mwakilishi Mohamed Ahmada, wa jimbo hilo, walisema wanaamini kuwa vikao hivyo vitaibua changamoto nyingi na kutambua zilizotatuliwa kwani zinahitaji kufanyiwa kazi.

Walisema changamoto kubwa ambazo  walizosikia katika shehiya mbali mbali ndani ya jimbo hilo ni ya kukosekana maji safi na salama, ambapo wananchi wa Mji Mkongwe wamelazimika kunywa maji ya chumvi, na kusababisha kupata maradhi ya vidonda vya tumbo kwa baadhi yao, babara za ndani  mbovu na kuingia maji  wakati mvua zinapo nyesha.

Changamoto nyengine walisema ni kuwepo kwa mazingira machafu  kunakosababishwa na wananchi kumwaga maji maji machafu na kutupa taka ovyo na makaro kujaa, kukosekana kwa ulinzi shirikishi.

Walisema tatizo jengine ni la  vijana kukosa ajira na kujishirikisha na vitendo viovu vikiwemo vya uvutaji bangi ,ulevi wa kupindukia na kujiingiza katika masuala ya wizi, kutakiwa kulipa kodi kubwa katika nyumba zao ambazo zinamilikiwa na Wakfu na Wizara ya Majenzi.