NA VICTORIA GODFREY

MZUNGUKO wa Pili wa mashindano ya Vijana walio chini ya umri ya miaka 17 unatarajia kuendelea leo kwenye uwanja wa Karume,Dar es Salaam.

Akizungumza na Zanzibar leo,Mkurugenzi wa Same Sports Investment ambao ni waandaaji wa mashindano hayo Mrisho Mamba, alisema maandalizi yamekamilika.

Alisema lengo la mashindano hayo ni kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana kutoka kwenye vituo vya michezo.

“Maandalizi yamekamilika na tunatarajia kuona ushindani katika mzunguko huu,kwani tunaamini timu zitakuwa zimejipanga vyema na kufanyika maboresho kasoro zilizojitokeza mzunguko wa kwanza,” alisema Mamba.

Mamba alisema lengo jingine ni kutoa nafasi kwa wamiliki wa vituo hivyo wapate sehemu ya kuangalia vipaji na namna wanavyowafundisha.

Alisema bingwa ataondoka na kombe,seti moja ya jezi, medali nafasi ya pili atachukua seti moja ya jezi ,wakati wa tatu ataondoka na mpira mmoja.