NA MWANAJUMA MMANGA
MBUNGE wa jimbo la Magomeni, Mwanakhamisi Kassim Said, ametoa msaada wa vitu mbali mbali kwa ajili ya kusaidia baraza la wazee la wilaya hiyo vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni moja.
Vifaa ambavyo alivikabidhi Mbunge huyo, kwa baraza la wazee la shehiya hiyo huko Magomeni Wilaya ya Mjini Unguja, ni pamoja na mipira ya maji, jezi za mpira na majora ya vitambaa vya sanda ya kuzikia.
.
Alisema lengo ni kuwashukuru wananchi baada ya kumaliza uchaguzi mkuu 2020 na kusikiliza changamoto zinazowakabili na wazee hao ambapo sanda itawasaidia wazee wale wanyonge waweze kuwasaidia.
“Nitawakabidhi Masheha hawa watano na kila sheha tutampa majora matatu ikiwa yote majora manane na mtu akifiwa sheha anatakiwa kumpa kitambaa cha sanda pamoja na pesa za ubani na zikimaliza waseme” alisema Mbunge huyo.
Mwanakhamisi alisema mpira wa maji kuna sehemu wananchi wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo, Hivyo utawasaidia kutatua kero hiyo kwa wananchi wale ambao wanatatizo la upatikanaji huduma ya maji safi na salama huku jezi za wanawake hivyo zitawasaidia kufanya mazoezi kwa timu mbili za wilaya hizo ikiwemo timu ya Mzalendo na Meya Juu.
Akizungumzia suala la usafi hivyo aliwataka wazee hao kuhakikisha wanadumisha mazingira katika maeneo yao, ili kuendana na Serikali ya awamu ya nane yenye lengo la kuhakikisha mji unakuwa safi.
Alisema iwapo wazee wakijikusanya pamoja wataweza kupata mikopo ya bei nafuu na kuondokana na changamoto zinazowakabili.
Nae Mwanaidi Abdalla Suleiman Katibu wa CCM jimbo la Magomeni, alisema ujio wao wamepata faraja kwa baraza la wazee kwa mashirikiano yao mbunge na mwakilishi ili kusikiliza chamgaoto zao zinazowakabili wazee hao na watahakikisha wanashirikiana kusikiliza kero za wananchi.
Mratibu wa jimbo hilo Faki Abdalla, ameushukuru sana msaada huo na kuwataka wananchi kutoa mashirikiano ya karibu na viongozi wa jimbo, ili huduma za maendeleo yanapatikana katika jimbo hilo.