NA VICTORIA GODFREY
TIMU ya Mchenga na Srelio zimeibuka washindi katika michezo yao ya ligi ya Kikapu ya Daraja la Kwanza (RBA) inayofanyika uwanja wa Bandari Kurasini,Dar es Salaam.
Mchenga iliibuka na ushindi baada ya kupata pointi 78–61 dhidi ya External katika mchezo uliochezwa juzi kwenye uwanja huo.
Katika robo ya kwanza External iliongoza kwa pointi 17-9, huku robo ya pili na ya tatu ilichukuliwa na Mchenga kwa kupata pointi 29-17,23-14 na robo ya nne External iliongoza kwa pointi 20-17.
Wafungaji waliong’ara kwa Mchenga Ethan Bully alifungwa pointi 17 akifuatiwa na Saudi Habibu pointi 17,wakati upande wa External wafungaji David Buberea aliongeza pointi 12 na Rigwa Gifion akiwa na pointi 11.
Mchezo mwingine ulikuwa Srelio ilishinda kwa pointi 66-54 dhidi ya Kigamboni.
Katika robo ya kwanza Srelio iliongoza kwa 17-15 robo ya pili walifungana 19- 19 wakati robo ya tatu na nne Srelio ilifunga 12-10 na 18-10.
Wafungaji wa Srelio Otto Bategeki aliongeza 20 akifuatiwa na Kenneth Mkindu pointi Tusa,wakati Kigamboni waliong’ ara ni Castro Teophil pointi 20 na Peter Levi aliongeza pointi 11.
Mchezo mwingine ulizikutanisha Patriot walioshinda kwa pointi 58-57 dhidi ya KIU.