MEXICO,MEXICO

RAIS wa Mexico Andrés Manuel López Obrador ameahidi kumpa hifadhi ya kisiasa mwanzilishi wa tovuti ya uvujishaji wa nyaraka za siri ya Wikileaks, Julian Assange, na kumsaidia kuachiwa huru.

Mahakama ya nchini Uingereza ilipinga kupelekwa kwa Assange nchini Marekani, kujibu mashitaka ya uhalifu wa kijasusi na kuvujisha siri za serikali.

Assange mwenye umri wa miaka 49 na ambaye afya yake imedhoofika, anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 175 gerezani ikiwa atapatikana na hatia.

Wakosoaji wanasema kesi dhidi yake ni kitisho kwa uhuru wa vyombo vya habari.