NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Chama cha Mpira wa Meza Tanzania ( TTTA) umekamilisha na kukabidhi Mpango mkakati na kalenda ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Michezo (BMT).

Akizungumza na Gazeti hili Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TTTA,Yahya Villu, alisema mpango mkakati huo, umeanisha mipango ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa mwaka huu.

Alisema wanakusudia kuwa na mashindano mengi ya ndani ili kuwapa uzoefu na kupima viwango vya wachezaji kwa kushiriki zaidi mafunzo ya uwamuzi na ukocha.

VIllu alisema kimataifa wanatarajia kuandaa mashindano mawili pekee mwaka huu yaliyowekwa kwenye kalenda

Alisema walibaini kuwa wachezaji hawana uzoefu wa kushiriki mashindano, hivyo wanajipanga upya kwa mashindano ya kimataifa yajayo.