NA MWANAJUMA MMANGA
MRATIBU wa Miradi ya elimu wa taasisi ya Milele Zanzibar Foundation, Ali Bakari Amani, amesema wanakusudia kutengeneza mitaala kwa ajili ya walimu waliopo maskulini ili kuimarisha ufundishaji wao na kuwa bora zaidi.
Amani aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili huko ofisini kwake Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar na kueleza kwamba hatua hiyo itasaidia kuomgeza ifamisi katika ufundishaji madasani, kuwapatia uwelewa ili kufanya vizuri mitihani yao ya darasani na kitaifa.
Alisema pamoja na kuwapa taaluma hiyo pia watapatiwa taaluma juu ya matumizi bora ya ITC ili kupata ujuzi wa ufundishaji kwa wanafunzi wakiwa darasani.
Alisema wanakusudia kutengeneza mitaala hiyo kama inavyoelekeza katika kuimarisha stadi za maisha, uimarishaji wa lugha ya kiengereza, masomo ya Sayansi, teknolojia pamoja na mafunzo ya ufundishaji wanafunzi wa kada mbali mbali ya masomo yao.
Aidha alisema utayarishaji wa mafunzo hayo kutakuwa na vikao mbali mbali vya wataalamu ili kuibua maeneo mahsusi ya mafunzo hayo pamoja na kueka namna ya kupima umahiri wa wanafunzi hao baada ya mafunzo.
Alisema hivi sasa wapo katika kutafuta wataalamu ambapo katika kufikia malengo ya Milele inakusudia kufanya kazi kwa ukaribu na wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na chuo Kikuu cha Taifa (SUZA).
Nae hatua hiyo nzuri itawasaidia kuongeza ujuzi katika kazi zao kutokana na hivi sasa dunia imekuwa inabadilika.
Hivyo kuna baadhi ya vitu vikiwa vinapafatana na vitu vinavyona na wakati uliopo hivyo taaluma hiyo itawaonyesha njia.