NA ABOUD MAHMOUD

MASHINDANO ya kuwania kombe la mapinduzi kwa mchezo wa mpira wa mikono (Handball), yameanza kwa kasi katika kisiwa cha Unguja  kwa kuzikutanisha timu mbali mbali za mchezo huo .

Katika uwanja wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Migombani majira ya saa 8:00 mchana timu ya Kwerekwe na Wete kutoka kisiwani Pemba zilivaana na Kwerekwe  kuondoka na ushindi wa mabao 31 -13 .

Mchezo mwengine ulipigwa majira ya saa 10:00 jioni kiwanjani hapo, baina ya KMKM na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Katika mtanange huo maafande wa JKU waliondoka uwanjani hapo wakiwa wanyonge baada ya kufungwa na waokoaji  wa KMKM mabao  29 – 20.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuendelea tena leo kwa kuzikutanisha timu za JKT na JKU majira ya saa 9:00 na saa 10:00 KMKM watavaana  na Nyuki.