NA JOSEPH NGILISHO, ARUSHA

MTOTO mwenye umri unaokadiriwa kuwa na miezi mitatu amekutwa amekufa kando ya nyumba kwenye migomba huku sehemu ya viungo vyake zikiwemo sehemu za Siri  vikiwa vimenyofolewa.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea mapema katika mtaa wa Lolovoni kata ya Sokoni 1,jijini Arusha baada ya mwili huo ambao jinsia yake halikufanyika mara moja kukutwa majira ya saa mbili asubuhi katika nyumba ya mkazi mmoja wa eneo Hilo.

Mwenyekiti wa mtaa huo,Orgeness Lema amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya ukatili kwa watoto yanayofanywa na  watu  wasio na hofu ya mungu.

“Niliigiwa simu nikiwa kanisani na kufika eneo la tukio nimeshuhudia mwili wa mtoto ukiwa kwenye migomba kando ya nyumba ya mkazi wa eneo hili ukiwa hauna miguu yote na mikono  na sehemu za Siri pia zikiwa hazipo nilitoa taarifa polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo “alisema Mwenyekiti

Aidha amesema kuwa serikali ya mtaa kwa kushirikiana na wananchi imeanza msako wa nyumba kwa nyumba ili kubaini nani amejifungua mtoto hivi karibuni na kwa sasa hana mtoto .

Naye balozi wa nyumba kumi katika mtaa huo,Omari Shedafa alisema kuwa alishuhudia mwili wa mtoto huyo akiwa uchi wa mnyama huku mikono na miguu pamoja na sehemu zake za Siri  zikiwa zimenyofolewa .

Naye Bibi mwenye nyumba ambayo mwili wa mtoto huyo umekutwa kando ya nyumba yake , Magdalena Shaushi Mkazi wa mtaa wa Lolovono alipata taarifa kwa watoto waliokuwa wakicheza kwenye migomba yake na alipofika alishuhudia mwili wa mtoto huyo na kutoa taarifa kwa balozi.

“Mimi nimeambiwa na watoto waliokuwa wakocheza kuwa Kuna mtoto ametupwa na nilipofika nimekuta mwili wa huyu mtoto akiwa Hana miguu na mikono Sasa sijui ni Nani amemtupa hapa kwenye nyumba yangu”alisema huyo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mjumbe wa serikali ya mtaa huo ,John Mchasu, amewataka wananchi kushirikiana kubaini aliyehusika na unyama huu, ili aweze kuchukulia hatua kwani kitendo hiki hakikubaliki.

“Ninachowaomba wananchi washirikiane na viongozi wa mtaa huu ili kufanya msako wa kuweza kubaini aliyehusika na kitendo hiki “alisema .

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Salumu Hamduni,, hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa

Mwili huo imehifadhiwa katika.hospital ya Mkoa Mount Meru kusubiri taratibu zingine za kiuchunguzi