NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya soka ya wazee wa Muembeladu imeondoka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wazee wa Buyu katika mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Buyu majira ya saa 10:00 jioni ambao ulikuwa wavuta nikuvute kwa timu hizo.

Hadi timu zinakwenda mapumziko Wazee wa Mwembeladu walikuwa wakiongoza na bao moja lililofungwa na Ally Iddi dakika ya 34.

Kurudi uwanja kumaliza kipindi cha pili timu hizo zilishambuliana kwa zamu kila mmoja akisaka nafasi ya kuingiza baa kwa mwenzake.

Dakika ya 56 Ramadhan Said wa timu ya wazee Muembeladu aliongeza bao la pili,huku bao la tatu likifungwa na Mohamed Issa dakika ya 67 na bao la nne lilimaliziwa na Kassim Abdalla dakika ya 89.