NA AMEIR KHALID
TIMU ya Muembemakumbi United imeitandika timu ya Fujoni Star mabao 4-0.
Mchezo huo ni mfulululizo wa ligi daraja la pili wilaya ya Kaskazini B uliopigwa uwanja wa Aluta Mangapwani.
Muembemakumbi ilitawala mchezo kwa vipindi vyote na kuwapa wakati mgumu wapinzani wao ambao walizidiwa kila idara.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika tayari Fujoni walikuwa wanaongozwa kwa mabao 3-0.
Mabao hayo yalifungwa na Ali Omar ‘Msauzi’ dakika ya 15, bao la pili lilipachikwa na Jailani Haji ‘Sanchez’ dakika ya 35 kwa penalti na la tatu lilifungwa na Hamiar Masoud ‘Costa’ dakika ya 36.
Kipindi cha pili Muembemakumbi iliendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la nne lililofungwa tena na Hamiar Masoud ‘Costa’ dakika ya 80.