KAMPALA,UGANDA

MGOMBEA urais wa NRM Rais Yoweri Museveni jana ameanza hatua zake za mwisho za kampeni wakati anarudi katika baadhi ya wilaya ambazo tayari amefanya kampeni.

Museveni ambaye anataka kuongeza utawala wake hadi muongo wa nne alisema ataanza kampeni yake kwa kukutana na viongozi wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) katika Wilaya ya Kisoro.

Katibu Mkuu wa chama cha NRM Justine Kasule Lumumba alisema kwamba Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu 1986 atarudi katika wilaya za Kisoro, Kassanda, Yumbe na Maracha ambapo atakutana na viongozi kadhaa wakati akizidisha kampeni zake.

Museveni alitarajiwa kufanya kampeni katika wilaya za Mukono,Wakiso na Kampala ambazo zilichaguliwa na tume ya uchaguzi .

Hata hivyo Lumumba aliwaambia waandishi wa habari kuwa kwa sasa wanashirikiana na tume ya uchaguzi kuwapa idhini ya kumrudisha mgombea wao kufanya kampeni.