NA ZAINAB ATUPAE

UONGOZI wa Jimbo la Malindi,umewataka wananchi wenye ulemavu shehiya ya Mchangani kujikusanya kwa pamoja na kuunda kikundi maalumu kwa ajili ya kufanya shughuli za ujasiria amali zitazowasaidia kupata kipato na kuendeleza maisha yao ya kila siku.

Wakizungumza na wananchi wa shehi hiyo hivi karibuni,walisema  katika kikundi hicho watawapa kipao mbele na kuhakikisha wanapata haki zao za msingi.

Mbunge wa Jimbo hilo, Suleiman Mohamed na Mwakilishi Mohamed Ahmda, alisema wamejipanga kutoa mitaji mbali mbali ikiwemo pesa na vifaa ambavyo watatumia kwenye kikundi chao watakacho kianzisha.

Mbunge huyo, aliwakabidhi vyombo mbali mbali katika kikundi cha Mchangani Cattering Services, vikiwemo  vya shughuli za maharusi na sherehe za kuzaliwa, huku akikabidhi laki 500,000 kwa kikundi cha wanachama wa baraza la wazee  cha Mchangani.