NCHI 39 zimeahidi kutoa dola milioni 439 kwa kipindi cha miaka mitano kwa mfuko wa Umoja wa Mataifa wenye lengo la kuimarisha amani katika nchi zilizoathiriwa na mizozo, kulingana na Umoja huo.

Kiwango cha fedha ambacho kinahitajika ni zaidi ya bilioni 1, 5, shirika la habari la AFP limebaini.

Kulingana na Marc-André Franche, ambaye anasimamia mfuko wa jjenzi wa amani ulioanzishwa mnamo mwaka 2006, “lengo kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano ni kufikia jumla ya dola bilioni 1.5”.

Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, mfuko huo umefadhili shughuli za kuilarisha amani katika nchi 51 (eneo la Sahel, Asia ya Kati, Amerika ya Kati, Balkan) kwa jumla ya dola milioni 356.

Nchi 38 zilichangia mfuko huo wakati wa mzunguko uliopita, lakini asilimia 60 ya pesa hizo zilizotolewa zilitoka kwa nchi tatu tu, Ujerumani, Sweden na Uingereza, kulingana na Marc-André Franche.