NA ZAINAB ATUPAE
TIMU ya soka ya New Version imeondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mchangani Star ikiwa ni muendelezo wa ligi daraja la pili Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mchezo huo uliotimua vumbi majira ya saa 10:00 jioni ambao ulikuwa wa ushindani.
Mabao ya New Version yaliwekwa wavuni na Khalifan Abdalla dakika ya tatu na bao la pili lilifungwa na Habib Khamis dakika ya 70.
Bao la kufutia machozi la timu ya Mchangani Star lilifungwa na Ali Omar dakika ya 44.