NAIROBI, KENYA

WAZIRI wa Afya nchini Kenya Mutahi Kagwe amesema kwamba Bima ya Afya ya Kitaifa NHIF itagharamia matibabu ya Ugonjwa wa Covid-19 kwa walimu. 

Kagwe alisema kwamba yoyote mwenye bima hiyo atanufaika na matibabu kupitia NHIF.

Alisema wameafikiana na Ofisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya huduma za walimu TSC kuwa NHIF itagharimia matibabu ya walimu na wanafunzi ambao wazazi wao walijisaliwa kwenye bima hiyo.

Kagwe aidha alisema Wizara ya Afya imetoa mwongozo wa kufanikisha kufunguliwa kwa taasisi za elimu ambao ulitumwa kwenye sekta zote zinazohusika.

Alisema japo kwa takribani wiki nzima viwango vya maambukizi vimekuwa chini ya asilimia tano,pana haja ya serikali za kaunti kuendelea kuimarisha mikakati ya kukabili maambukizi zaidi na kuwahudumia waathiriwa.