ANKARA,Uturuki

KIUNGO wa kati wa Arsenal Mesut Ozil ameanza mazoezi baada ya kukamilisha mchakato wa kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki.

Mchezaji huyo, 32, aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani alijiunga na Gunners kutoka Real Madrid kwa pauni milioni 42. 4 mwaka 2013.

Alishinda makombe ya FA akiwa na Arsenal na kufunga mabao  44 katika mechi zote 254 alizoshiriki lakini bado hajaichezea timu hiyo tangu mwezi Machi.

“Ningependa kuishukuru klabu kwa safari hii nzuri katika kipindi cha miaka  saba ,” Ozil amesema.

“Ni vigumu kwangu kuandika kwa maneno upendo nilio nao kwa klabu hii na mashabiki wangu,” Ozil amesema katika barua ya wazi.

“Naweza kutoa shukrani zangu kwa miaka minane katika barua moja tu?

Ameongeza kuwa: “Arsenal klabu yenye hadhi yake na heshima, kitu ambacho kila wakati huwa ninakihisi nikiwa uwanjani.”Kanuni za hadhi, heshima na adhima havistahili kusahaulika. Ni jukumu la kila mmoja katika klabu kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili haya.