LONDON, England
KIUNGO, Mesut Ozil, amesema, hana nia ya kustaafu atakapoondoka Arsenal, na upendeleo wake ni kuhamia Fenerbahce au Ligi Kuu ya Soka ya Marekani.
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani yuko kwenye siku za kufa za kazi yake na Arsenal, akiwa ameganda kabisa kwenye picha na meneja, Mikel Arteta.
Ozil hajajitokeza Arsenal tangu Machi, licha ya kuendelea kuwa ‘fiti’ na anapatikana kwa uteuzi, na ni swali la kuwa ataondoka Januari au mwishoni mwa msimu.
Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid amekuwa katika hali nzuri kwenye mitandao ya kijamii wakati wa kukosekana kwake uwanjani, na alifanya kikao cha maswali na majibu kwenye ‘twitter’ juzi.
Alijibu maswali kwenye mada anuwai, na moja ikiwa kwamba hakujuta kwa kujiunga na Arsenal.
Ozil pia aliulizwa ikiwa ana mpango wa kustaafu atakapoondoka Arsenal, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 hakuwa na shaka katika majibu yake.
“Nitafanya hivyo,” alisema alipoulizwa ikiwa angecheza baada ya kuondoka Arsenal. “Kuna nchi mbili ambazo ninataka kucheza mpira kabla ya kustaafu: Uturuki na Marekani.
“Ikiwa nitakwenda Uturuki, nianweza tu kwenda Fenerbahce”.
Maoni ya Ozil yanaongeza tu mafuta kwenye moto kuhusu kuhamia Fenerbahce.
Miamba hiyo ya Uturuki imekuwa ikihusishwa vikali na mpango wa kumchukua Ozil, na ikidaiwa kuwa mpango unafanywa kwa yeye kuelekea klabuni hapo Januari.Mapema katika maswali na majibu yake, Ozil alizungumzia vyema juu ya uhusiano ambao anao na Fener.