NA MADINA ISSA

BENKI wa Watu wa Zanzibar (PBZ), imesema katika kuunga mkono serikali ya awamu ya nane kupitia sera yake ya kuimarisha Uchumi wa Buluu inaendelea kutoa elimu kwa wananchi na wateja wao.

Ofisa Masoko Mfawidhi wa Benki ya PBZ, Mohamed Khamis Ismail, aliyasema hayo akizungumza na Zanzibar Leo, katika Uwanja wa Maisara Mjini Unguja, ambapo alisema wateja wao watanufaika kwa kupata mkopo wa vitendea kazi ikiwemo matrekta.

Alisema huduma hiyo sio mpya kwa benki bali wananchi hawaifahamu vizuri, ila waliweza kufahamisha na wateja wengi kuhamaisha kujiunga na huduma hiyo kwani itawanufanisha katika shughuli za uvuvi, uvunaji wa mazao ya habari, ili kwenda sambamba na uchumi wa buluu.

Akizungumzia maonesho ya saba Afisa huyo alisema kuwa maonesho hayo yamekwenda vizuri licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo ambapo wananchi wamekuwa wakijitokeza kufuata huduma katika banda lao.

Alisema changamoto kubwa iliyojitokeza katika maonesho hayo kwa PBZ ni wateja wao kutofahamu lengo na madhumuni ya maonesho hayo ambapo wengi wao walijua kuwa wanakwenda kuoneshwa bidhaa na sio kununua bidhaa.