NA MWAJUMA JUMA
KOCHA wa timu ya soka ya Polisi Yussuf Ramadhan Khamis ‘Sape’, amesema haikuwa rahisi kuifunga KMKM kutokana na uwezo wao ikilinganishwa na timu yake.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Sape alisema kitu ambacho kiliwasaidia kupata ushindi, ni kuwa na nidhamu ya hali ya juu ya mchezo kwa kujipanga vyema katika safu ya ulinzi na kushambulia kwa kushtukiza.
Hivyo alisema hatua hiyo imewafanya watimize lengo lao na kufanikiwa kuibuka na ushindi.
“Hali kama ulivyoiona na ilikuwa ngumu sana lakini tulimuomba Mwenyezi Mungu na tunashukuru alitupa tulichokihitaji, KMKM ni wazuri katika idara zote kulinganisha na timu yetu”, alisema.