NEW YORK,MAREKANI

MWENDESHA mashitaka katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani amesema polisi mzungu aliyempiga risasi saba mgongoni kijana mweusi Jacob Blake mwezi Agosti mwaka jana hana mashitaka ya kujibu, kwa sababu alikuwa na haki ya kujilinda.

Uamuzi huo ulikosolewa mara moja na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na pia baadhi ya maofisa wa serikali, na hali hiyo inatishia kutokea maandamano mapya.

Gavana wa jimbo hilo Tony Evers ambaye ni kutoka chama cha Democratic alisema uamuzi huo ni ushahidi kuwa bado ipo kazi kubwa kuweza kufikia usawa wa watu nchini Marekani, naye msaidizi wake Mandela Barnes ambaye ni mweusi.

Alisema ameshitushwa na uamuzi huo aliouita, tusi kwa mfumo wa haki.

Jacob Blake alipooza sehemu ya chini ya mwili wake kutokana na risasi hizo alizomiminiwa tarehe 23 Agosti mwaka 2020.