NA MARYAM HASSAN

WAKILI wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Ayoub Nassor, ameiomba mahakama kuahirisha kesi inayomkabili mshitakiwa Alawi Ramadhan Sudi (34) mkaazi wa Bububu, kwa sababu haina dhamana.

Wakili huyo alitoa ombi hilo mbele ya Hakimu wa mahakama ya mkoa Mwera, Said Hemed Khalfan, wakati jalada hilo lilipofikishwa mbele yake na kusomewa mshitakiwa huyo.

Alisema licha ya kuwa mshitakiwa ameomba apatiwe dhamana, mahakama itupilie mbali ombi la mshitakiwa huyo kwa sababu kosa lake ni miongoni mwa makosa ya jinai na halina dhamana.

Badala yake, ameiomba mahakama kuahirisha shauri hilo na kupangwa tarehe nyengine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ushahidi, kwa sbabu tayari upelelezi wake umekalimika.

Mapema alimsomea shitaka lake mshitakiwa huyo, kwamba alitenda kosa la kubaka na kutorosha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa, huku akijua kuwa ni kosa kisheria.

Kosa la kutorosha anadaiwa kutenda April 18, 2019 majira ya saa 11:30 za jioni huko Kibele wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.

Mshitakiwa huyo bila ya halali, alimtorosha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa (jina linahifadhiwa na gazeti hili) ambae yupu  chini ya uangalizi wa wazazi wake na hajaolewa, kutoka njiani wakati akitokea dukani  na kumpeleka kwenye nyumba huko huko Kibele kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Baada ya kumtorosha mshitakiwa huyo anadaiwa kumuingilia mtoto huyo kinyume na maumbile, kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 13 (a) cha sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

Tukio anadaiwa kutenda siku hiyo hiyo majira ya saa 1:30 za usiku huko Kibele wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja, alimuingilia kimwili kinyume na maumbile mtoto huyo kitendo amacho ni kosa kosheria.

Baada ya kusomewa shitaka lake mshitakiwa huyo alikataa na kuiomba mahakama kumpa dhamana, kitendo ambacho kilikataliwa na upande wa mashitaka.