NA VICTORIA GODFREY

Uongozi wa Tanzania Prisons umesema umejipanga kufanya vizuri ili kupata pointi tatu dhidi ya Mawenzi katika mchezo wa Kombe la FA utakaochezwa Januari 6 mwaka kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga mkoani Rukwa.

Akizungumza na Zanzibarleo,Katibu MKuu wa Prisons ,Ajabu Kifukwe,alisema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri.

Alisema kuwa wachezaji wapo tayari na fiti kutumia uwanja wa nyumbani vyema ili kubakiza pointi tatukwa za wapinzani wao.

“Maandalizi yanaendelea vizuri chini ya Kocha Salum Mayanga kuhakikisha wachezaji wanajipanga kikamilifu waweze kutimiza malengo,” alisema Kifukwe.

Kifukwe alisema kuwa wanatambua wapinzani wao wanajipanga kupata matokeo mazuri,lakini watapambana kufa au kupona kuhakikisha ushindi unabaki nyumbani.

Alitoa mashabiki wa Rukwa kujitokeza kwa wingi kutoa sapoti ya kuwashangilia I’ll kuwapa nguvu wachezaji kuonyesha uwezo na ushindani katika mchezo huo.