NA MWANDISHI WETU

TANZANIA Prisons ikiwa Uwanja wa Nelson Mandela imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wa mzunguko wa pili.

Kipindi cha kwanza timu zote mbili zilitoshana nguvu bila kufungana ndani ya dakika 45 za mwanzo za mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Kipindi cha pili,Prisons walianza kupata bao dakika ya 52 kupitia kwa Jumanne Elifadhili.

Bao la kuweka usawa kwa Yanga lilifungwa na Saido Ntibanzokiza dakika ya 76 katika harakati za kuweka mzani sawa ndani ya uwanja.

Yanga imefunga mwaka 2020 ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 bila kupoteza.

Hili ni bao la pili kwa Ntibanzokiza ambaye ni ingizo jipya, bao lake la Kwanza alifunga mbele ya Dodoma Jiji.

Sare hiyo unaifanya Yanga kufikisha pointi 44 ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya Kwanza baada ya kucheza mechi 18, Tanzania Prisons inafikisha pointi 22 ikiwa nafasi ya 9.