KINSHASA,DRC

RAIS Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amekutana  na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi.

Rais Tshisekedi alisema jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo inathamini urafiki kati yake na China na iko tayari kuendeleza zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Pia alisema DRC inaishukuru China kwa msaada wake kwenye mapambano dhidi ya janga la COVID-19 na maendeleo ya uchumi wake.

Baada ya mazungumzo, nchi hizo zilisaini hati ya maelewano kuhusu ushirikiano wa pendekezo la ukanda mojana njia moja.

Wang Yi alisema Ukanda moja,Njia moja ni pendekezo muhimu la ushirikiano wa kimataifa lenye lengo la kuhimiza mafungamano ya kiuchumi kati ya nchi,kuunganisha mikakati ya maendeleo, kuendeleza juhudi za pamoja, ili kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja.