NA JOSEPH NGILISHO, ARUSHA

MKUU wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta ameiagiza Mamlaka ya Mapato  mkoani humo (TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwafuatilia watu wote wanaostahili kulipa kodi na kuhakikisha wanalipa.

Kimanta alitoa agizo hilo jana wakati akifungua kikao Cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) ambapo alisema kuwa ukusanyaji wa kodi ni lazima upewe kipaumbele katika mkoa huo, ili maendeleo yaweze hupatikan katika sekta zote.

Alisema kuwa wakikusanya kodi kwa wingi wanaijengea serikali uwezo wa kutengeneza miundombinu ya vituo vya afya, barabara, maji shule na mengineyo hivyo wale wote wanaostahili kulipa kodi ndani ya mkoa wa Arusha walipe.

“Natoa maelekezo kwa Meneja wa TRA mkoa wa Arusha ashirikiane na Kamanda wa TAKUKURU mkoa kuwafuatilia wote wanaostahili kulipa kodi na kuhakikisha wanalipa, tunataka kodi,”Alisema Kimanta.

Alifafanua kuwa hakuna haki bila wajibu hivyo ukusanyaji wa kodi ni lazima, kwani ikilipwa wanaijengea serikali uwezo wa kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Aidha kwa upande wa elimu alisema kuwa

elimu mkoa wa Arusha unaongoza kitaifa ambapo katika matokeo ya kidato cha nne na kidato cha pili imeongoza kitaifa  huku upande wa afya ukiwa ya pili kwa suala la lishe ikifuatiwa na kigoma.

Alieleza mafanikio hayo yametokana na mshikamano mkubwa walionao unaowafanya wafanikiwe hivyo ni rai yake kuwasihi viongozi wa sekta zote kuendeleza mshikamano huo kwa kuwa wamoja, kupendana ukiwa ni pamojan na pale lenye changamoto kurekebisha kwa haraka.

Alisema katika wilaya zote sita Kuna upungufu wa madarasa  126 ambapo anawashukuru wakuu wa wilaya na wakurugezi kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kuhakikisha ya kujenga madarasa kea kushirikiana na wananchi na hadi kufika Februari 28 upungufu huo utakuwa umeondoka.

“Lazima madarasa yajengwe na nilazima kasi iongezeke ili pasiwepi na wanafunzi watakaoshindwa kusoma Kutokana na ukosefu wa miundombinu ya madarasa,” Alisema Kimanta.

Aliendelea kusema kuwa mkoa wa Arusha mpaka sasa upo shwari na vyombo vya usalama vinatekeleza wajibu wake kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza .