ZASPOTI
MWANASOKA wa Ureno na klabu ya Juventas, Christiano Ronaldo, amezidi kuandikisha historia na kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mtu wa kwanza duniani kufikisha wafuasi milioni 250 katika mtandao wa Instagram.


Ronaldo hivi karibuni alijinyakulia tuzo ya mchezaji bora wa karne hii.
Nyota huyo aliyewahi kuzichezea Manchester United na Real Madrid, sasa yupo nchini Italia akikipiga na Juventus ambayo inafanya vizuri na imekua ikitegemea huduma zake.


Mara kadhaa Ronaldo amekua akishindanishwa na nyota wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi ambae pia anaendelea kung’ara akiwa na tuzo sita za Ballon d’Or.(AFP).