UTAWALA wa miaka minne wa rais wa Marekani Donald Trump umefikia ukingoni baada ya rais huyo kushindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo Novemba 4 mwaka jana.
Trump alisababisha figisu figisu kadhaa baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu na Joe Biden ambaye ni makamu wa rais wa zamani wa Marekani aliyehudumu wakati wa Barack Obama.
Chini ya sera yake ya ‘Marekani kwanza’, Trump alionekana kama kuitenga nchi yake na ulimwengu ikiwemo kusababisha hasama na badhi ya mataifa rafiki wa ndani wa ndani wa Marekani.
Tump alishuhudiwa akifanya mabadiliko kadhaa ya kisera na kisheria kwenye mipango kadhaa iliyoasisiwa na mtangulizi wake Barack Obama kwa ajili ya wananchi wa Marekani.
Baadae alivuka mikapa na kuingilia sera ya nje ya Marekani ambapo alishuhudiwa akiazisha vita vikubwa vya kibiashara baina ya taifa hilo na China na baadhi ya nchi nyengine duniani, hali ambayo ilionekana kuathiri sana uchumi wa dunia.
Kwa sasa Marekani inaingia kwenye enzi za utawala mpya chini ya Joe Biden, ambaye atashika usukani akiwa rais wa awamu ya 46, huku akielezwa kuwa ndiye rais atakayeweka historia kwa mara ya kwanza nchini Marekani kuwa na umri mkubwa ambapo kwa sasa ana umri wa miaka 78.
Wakati Biden anaingia madarakani suali kubwa linalotarajiwa kutathminiwa na walimwengu je rais huyo mpya atachukua msimamo gani wa kisera dhidi ya eneo tete duniani la mashariki ya kati?
Trump ambaye tayari ameshafungasha virago na kuondoka ikulu ya ‘white house’, aliochukua mkondo wa kuwabeba mno nchi maswahiba katika eneo la mashariki ya kati kiasi cha maswahiba hao wa Marekani kutamba sana.
Hatua za Trump kwneye mizozo kadhaa ya eneo la mashariki ya kati kama Israel, na Palestina, Yemen, Iraq na hata katika eneo la Afrika Kaskazini zimekosolewa vikali, hivyo hatutashanga kumuona Biden akifanya mabadiliko makubwa.
Trump akiwa hivi karibuni akiwa amebakisha siku chache kuondoka madarakani utawala wake ulifanya maamuzi ya haraka ya kuimarisha mipango ya sera yake ya kigeni katika Masharikii ya Kati.
Hivi karibuni utawala huo wa Trump uliwaorodhesha waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoaidiwa na Iran kuwa kundi la kigaidi na kuwaekea vikwazo maofisa wa kadhaa wa kijeshi wa Iran na mashirika kadhaa ya Iran.
Maamuzi mengine ya kisera yaliyofanywa katika muda wa mwisho wa utawala wa Trump ni pamoja na kuliiidhinisha na kulitambua rasmi eneo linalogombaniwa la Sahara Magharibi kuwa himaya ya Morocco.
Hatua hizi zote zimetumika kuitenga Iran na kuimarisha uwezo wa taifa la Israel katika kanda hiyo, hatua ambazo wapiga kura wengi wa Marekani huenda wakakubaliana nazo.
Lakini pia maamuzi hayo ya karibuni yamekosolewa vikali. Lakini utawala unaoingia wa Biden utaweza kuyabatilisha maamuzi hayo ambayo yanasemekana kuwa na madhara makubwa, na je, itachukua muda gani na mchakato utakuwa mgumu kiasi gani?
Marina Henke, Profesa wa mahusiano ya kimataifa katika taasisi ya Hertie, mjini Berlin, alisema kinadharia, baadhi ya mabadiliko yanaweza kuwa rahisi kufanyiwa mabadiliko na rais mpya wa Marekani Joe Biden.
Akitoa mfano, Marina alisema uamuzi kuhusu Morocco na Sahara Magharibi ulikuwa katika aina ya tangazo lililofanywa na Trump, hata hivyo tangazo hilo halina nguvu za kisheria isipokuwa kama bunge la Marekani litaidhinisha na linaweza kubatilishwa kwa urahisi na tangazo jingine kutoka kwa rais mpya.
Mtaalamu huyo alisema amri za rais matamko hufanya kazi katika njia hiyo hiyo, ambapo yanaweza kufutwa kiurahisi sana na rais mpya Joe Biden.
Aidha kulitangaza kundi fulani kuwa la kigaidi ni kitu kigumu, lakini sio sana. Waziri wa mambo ya kigeni lazima atangaze nia yake ya kufanya hivyo, kisha bunge lina siku saba kuwasilisha malalamiko yoyote.

Henke alisema waziri anayeondoka wa mambo ya kigeni Mike Pompeo alitengeneza dhana kuhusu masuala tete ya sera za kigeni yenye umuhimu kwa wapiga kura wa Marekani.
Masuala hayo ni kama yanayoihusisha Iran, China na Cuba. Na kama Biden atachukua hatua za haraka, Warepublican wanaweza kulalamika kuwa ana nia ya kuzungumza na magaidi.
Mahusiano ya nchi za kiarabu na Israel yanaungwa mkono na pande zote, lakini huenda kukawa na baadhi ya sera za kigeni zilizowekwa na utawala wa Trump ambazo uongozi mpya wa Marekani hasingepanda kuzifuta.
Julian Barnes-Dacey, mkurugenzi mtendaji wa mpango wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Baraza la Ulaya kuhusu mahusiano ya kigeni, alisema kuanzishwa mahusiano ya nchi za Kiarabu na Israel ni kitu ambacho kinaungwa mkono na pande zote za kisiasa.
Hata hivyo, kuhusu hali ya kiutu nchini Yemen, Biden huenda akajaribu kutafuta mbinu ya suala hilo badala ya kulikabili moja kwa moja.
Profesa wa masuala ya usalama katika chuo kikuu cha Massachussettes, Lowell nchini Marekani alisema yote hayo yanahusu dhamira ya kisiasa. Amri za rais zinaweza kutolewa na kutekelezeka haraka. Bunge halihitaji kuhusika.
Hata hivyo kama unazungumzia mataifa kama vile Iran au Syria, au baadhi ya wahusika nchini Iraq hilo litakuwa suala gumu.
Ian Black, msomi mwandamizi katika kituo cha Mashariki ya Kati cha Chuo cha Masuala ya Kiuchumi mjini London alisema suala muhimu ni kurejea katika mkataba wa nyuklia wa Iran.
Alisema shinikizo kuhusu suala hilo ni kubwa mno, hata ingawa utawala wa Trump ulifanya kazi kubwa kuyaunganisha mataifa ya Ghuba na Israel dhidi ya Iran. Watalaamu tayari wameonya kuwa muafaka wa Iran utachukua muda kufufuliwa.