NA KASSIM SALUM

MASHIRIKA pamoja na taasisi binafsi nchini zimeshauriwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya nane kwa kutoa misaada mbali mbali itakayosaidia kuimarisha ustawi wa watendaji na jamii kwa ujumla.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Shaaban Seif Mohamed, ametoa wito huo wakati akipokea msaada wa mito ya kukalia  iliyotolewa na taasisi ya ‘helping hand for relief and development’ ya Marekani.

Katibu Shaabani, aliishukuru taaisi ya Muzdalifah pamoja na heling hand ya Marekani kwa jihada wanazochukua katika kutoa misaada mbali mbali inayolenga kuisaidia jamii hawa kwa kuwafikia watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Alieleza kuwa mito hiyo mia tatu (300) iliokabidhiwa  itagaiwa katika taasisi za serikali, ili kufanikisha lengo lililokusudiwa la kuwaasaidia watendaji wa serikali kuweza kuongeza ufanisi katika sehemu zao za kazi sambamba na kuimarisha Afya zao.

Akikabidhi mito hiyo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Muzdalifah Farouk Hamad, iliyotolewa na taasisi ya Helping hand for relief and development ya Marekani, amesema jumuiya yao imeona umuhimu wa kukabidhi  mito hiyo kwa watendaji wa serikali kutokana na kutumia muda mwingi kukaa katika viti wakiwa wanatekeleza majukumu yao hali inayotishia usalama wa afya zao.

Farouk alifafanua kuwa kitendo cha mfanyakazi kutumia muda mrefu kukaa katika kiti kitaalamu kinaweza kumsababishia kupata matatizo ya uti wa mgongo hivyo taasisi yao imeona ipo haja ya kutoa msaada huo utakaosaidia kuondosha changamoto hiyo.

Aidha alishukuru serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dk. Husssein Ali Mwinyi, kwa Dhamira ya dhati ilionayo katika kuzisaidia taasisi binafsi kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kontena iliobeba mzigo huo.

Amesema  taasisi yao imepata msamaha wa kodi kwa kontena ishirini (20)  zinazotarajiwa kuingia nchini mwezi Aprili mwaka huu, zikiwa na vifaa tiba, vyakula, nguo na vifaa vya kuwasaidia watoto katika  skuli mbali mbali za Zanzibar.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka kampuni ya misaaada ya kimarekani, ya helping hand for reliefanda development, Hassan Kimbwembwe, ameendelea kuishukuru serikali ya Zanzibar kwa kuendelea kuziamini taaasisi binasfsi kwa juhudi wanazozifanya kwa kuisaidia serikali, hata kufikia kusamehe kodi kwa mizigo inayoingia nchini.

Jumla ya mito 300 imetolewa na taaisi ya Muzdalifah kwa msaada wa helping hand kwa ajili ya kusambazwa kwa watendaji wa ofisi za serikakli.