RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akipokea maandamano ya wananchi wakati wa kilele cha Sherehe za miaka 57, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika jana katika viwanja vya Mnazimmoja Mjini Unguja.
KIJANA mwenye ulemavu akihudhuria katika kilele cha Sherehe za miaka 57, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika jana viwanja vya Mnazimmoja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, wa kwanza kushoto, akipokea maandamano ya magari ya jeshi la wananchi wa Tanzania, katika kilele cha Sherehe za miaka 57, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
ASKARI wa vikosi vya SMZ wakipita kwa maandamono mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, (hayupo pichani) katika kilele cha Sherehe za miaka 57, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
MAKAMU wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluh Hassan, (kulia) Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi, Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Mama Fatma Karume, na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, wakiimba nyimbo ya mashujaa katika kilele cha Sherehe za miaka 57, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, (katikati) akisubiri kupokea maandamano ya wananchi wakati wa Sherehe za miaka 57, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika jana katika viwanja vya Mnazimmoja Mjini Unguja. (PICHA NA ABDALLA OMAR).