NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kwenye mchezo wao dhidi ya FC Plutnum.

Afisa Habari  na Mhamasishaji wa klabu hiyo Hajji Manara, alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Serena Hotels.

Mchezo huo wa marudiano utachezwa kwenye Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam saa 11:00 jioni.Ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Zimbabwe Simba walipoteza kwa bao 1-0.

Alisema wamepata majibu ya barua yao kuwa wameridhiwa na CAF mechi kuwa saa 11:oo jioni wakati awali ilipangwa saa 1:00 usiku.

Hajji alisema waliomba hivyo wakiangalia miundo mbinu ya Dar es Salaaam ili Watanzania wengi wapate fursa ya kuangali mechi hiyo.

 “ Platnums wao wanaendelea na maandalizi kesho watafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkapa,” alisema

Viiongilio kwenye mchezo ni 5000 kwenye mzunguko badala ya  7000 ,  VIP B na C ilikuwa 20000 imeshuka hadi 15 VIP A 40000 na Plutnums 150000 hazina punguzo.

Aidha Hajji alisema lengo  la kupunguza viingilio nikuvutia watu kwenda kwa wingi uwanjani , ambapo wanatamani kuona idadi ya watu inaongezeka.