NA MWAJUMA JUMA

KLABU za soka za Yanga, Simba na Namungo zitashuka dimbani leo kucheza michezo yao ya kombe la mapinduzi.

Yanga inashuka kuumana na Namungo mchezo ambao utachezwa saa 2:00 usiku, wakati Simba itashuka majira ya saa 10:00 kuumana na Chipukizi.

Simba na Namungo wao watakuwa ni mechi zao za kwanza wakati Yanga itakuwa wa pili baada ya juzi kucheza na Jamhuri.

katika mchezo huo Yanga ilitoka sare ya kutokufungana mchezo ambao ulikuwa na upinzani wa hali ya juu.

Awali Simba ilikuwa ishuke dimbani jana Januari 7, lakini kutokana na kukabiliwa na mchezo wake wa kimataifa mechi hiyo ilisogezwa mbele.

Simba imepangwa kundi B pamoja na Mtibwa ambao ndio wanaoongoza kwenye msimamo kwa kuwa na pointi tatu baada ya mchezo wake wa kwanza kuifunga Chipukizi bao 1-0.