NA KHAMISUU ABDALLAH

Kwa watu wengi wa Zanzibar siku ya Ijumaa ya tarehe 25 Disemba, mwaka jana, haisahauliki katika historia HIVI karibuni jengo maarufu la kihistoria yao.

Hii ni siku ambapo moja ya majengo maarufu Visiwani na Afrika Mashariki liliobeba historia ya aina yake, Beit el Ajaib (Nyumba ya Ajabu) lilipopoporomoka eneo kubwa na kusababisha maafa.

Watu wawili walipoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa wakati jengo hilo lilipoporomoka wakati wakiwa katika harakati za kulifanyia ukjarabati.

Akizungumza kwa sauti ya chini akiwa katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja akipata matibabu, mmoja wa watu aliyenusuurika na kujeruhiwa, Hamad Matar Abdalla, alisema anachokumbuka ni kuwepo pamoja na wenzake katika jumba hilo wakilifanyia matnegenzo akama walivyoelekezwa na wataalamu.

Alisema siku hiyo wakati akiwa kazini alisikia mshindo mkubwa na bada ya  hapo hakufahamu kilichotokea mpaka alipopata fahamu na kujikuta akiwa hospitali.

Hamad aliepata majeraha ya mbavu na vidole vitatu vya mkono kukatika kutokana na kuporomokewa na ukuta wa jengo

Vile vile amevunjika bega la upande wa kushoto na hali yake imekuwa inaendelea vizuri.

Nae Ali Ramadhan Juma ambaye alijeruhiwa na kuwa hana fahamu alipofikishwa hospitali amesema hali yake.

Ali ambae ni majeruhi wa mwanzo kuokolewa katika ajali hiyo aliumia kichwa.

Akizungumzia kilichotokea siku ile wakati akiwa kazini anasema siku ya tukio alikuwa kazini na wenzake sita, lakini wakati akiwa anaendelea, lakini hakumbuki kilichotokea isipokuwa kujikuta yupo hospitali ya Mnazimmoja.

Kama wenzake wengine waliojeruhiwa aliipongeza serikali kupitia Wizara ya Afya kwa jitihada kwa kuwapatia huduma muwafaka na kwa wakati na kupelekea hali zao zinaendelea vizuri.

Wakatri nilipookuwa ninazungunza na wale ambao walikuwa wamepata nafuu wagonjwa wengine walikuwa wamewekwa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU).

Nao ni Haji Juma Machano (37), mkaazi wa Chumbuni na Dhamir Salum Dhamir (37) wa Kinuni.

SIMULIZI ZA WALINZI WALIOSHUHUDIA JENGO LIKIANGUKA

Walinzi  ambao walikuwa hapo na kunusurika wakatri jengo lilipoporomoka wamesema kuanguka kwa jengo hilo daima kutabakia katika kumbukumbuka zisisahaulika za maisha yao.

Walinzi hao ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya Garda Security walisema mporooko wa hilo jengo ulikuwa wa kutisha na yeye na wenzake walionusurika walipata mshituko mkubwa hasa walipogundua kwamba wenzao wawili walishaiaga dunia.

Shamte Mohammed Shamte alisema aliyoyashuhudia siku ile abadan hatayasahau.

Alisema kwa masiku kidogo eneo lilioporomoka hilo jengo lililikuwa na ufa ambao ulikuwa ukidondosha mchanga.

“Kila siku tulikwenda kuuangalia ule ufa na kukuta unaendelea kudondosha mchanga, lakini siku ya tukio kasi ya mchanga kuporomoka ilizidi. Hali hii ilitupa wasi wasi mkubwa,” alisema.

Alisema walipoona jengo linataka kuporomoka walitimua mbio huku wakipiga kelele hadi walipofankiwa kutoka nje huku na kuwataka wenzao waliokuwemo ndani kutoka kwa kuwaambia jengo lilikuwa linaporomoka.

Wenzao wakaacha kila kitu na kukimbilia nje kunusuru maisha yao.

Siku hiyo waliokuwa kazini pamoja na wenzao walikuwa watu 16, lakini ni 12 tu ndio waliofanikiwa kutoka nje salama.

“Mungu alitupenda sana kwani siku za kazi wafanyakazi huwa kati ya 40 na 50. Hii ni mbali ya wale ambao hawajisajili katika buku la mahudhurio. Lakini siku ile ilikuwa sikukuu na

Kama jengo lingeanguka siku ya kazi huenda maafa yangekuwa makubwa, alisema.

Aziz Nassor Ahmada alisema wakati jengo lilipoanza kuporomoka wafanyakazi waliokufa na kujeruhiwa walikuwa upande wa kulia wa jengo na wale waliokuwa upande wa kushoto nadio walitoka salama.

Wakati jengo la Beit al Ajab lipoanguka eneo la chini halikuwa katika hali nzuri na sehemu hio ilikuwa likuwa ikiporomoka mara kwa mara.

“Jengo lilipokuwa linaporomoka tulipiga kelele za kutahadharisha wenzetu na kuwataka washuke. Kwa bahati mbaya wenzetu waliokuwepo juu hawakuwahi kwa sababu ngazi za kushukia zilikatika na kuwakwamisha wanne waliokuwepo juu ya mnara,” anasema.

Alisema kabla ya kuanguka jengo lilidata madirisha na kuashiria hali siuo nzuri.

Aziz akizungumzia vifo Pande Haji Makame (39) mkaazi wa Bumbwini, Mkoa wa Kaskazini Unguja, na Buruhani Ameir Mavuno (25) mkaazi wa Daraja bovu alisema yeye na wenzake waliokuwepa katika ghorofa iliyoporomoka walifukiwa na kifusi na kupelekea kupoteza maisha.

“Kabla ya tukio wenzetu walipoteza maisha tulijuliana hali kabla ya kuanza kazi, kumbe ilikuwa ndio wanatuaga., Inasikiisha”, alieleza huku akitikisa kichwa.

Waliipongeza serikali kupitia vikosi vyake, kikiwemo cha Zimamoto na Uokozi kwa kwa kufika hapo mapema na kufanikiwa kuwaokoa wenzao wanne wakiwa hai.

VIONGOZI WA SERIKALI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, akimpa pole Hamad Matar Abdalla (39) mmoja wa majeruhi wa ajali ya jengo la ghorofa la Makumbusho la Beit al Ajaib lililoporomoka na kuua wayu wawili Zanzibar.

Mara tu baaada ya jengo viongozi wengi, akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdullah, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Lela Mohammed Mussa walifika hapoo.

Vile vile waliwazuru majeruhi hospitali na kwenda kutoa mkono wa pole kwa familia zilizopoteza watu wao na kzungumza na wadau mbalimbali wa Mji Mkongwe.

Rais Mwinyi alisema Zanzibar imepoteza nembo yake muhimu ya kihistoria na haiba ya mji wa Zanzibar na kuelezea umuhimu wa kufanywa juhudi za haraka katika kuurejesha urithi huo, kuwa na mpango maalum wa hifadhi.

Alisema serikali itaweka kipaumbele katika uhifadhi wa Mji Mkongwe, kuwa na bajeti yake katika uhifadhi, kuwa na wafanyakazi wenye taaluma na kuanzisha mfuko maalum.

Alisema Mji Mkongwe sio urithi wa nchi pekee bali ni wa duniana kwahivyo ni lazima kufanya kila jitihada kuhakikisha unatunzwa.

Alisisitiza  kwamba kama serikali haijachukua hatua itapelekea kila siku kutokea kwa matatizo  yanayoweza kuepukika.

Aliwataka wadau kushirikiana katika kutafuta njiaza kuepusha ajali na kuangalia mustakabali mzima wa mji huo.

Dk. Mwinyi aliunda tume ya uchunguzi katika kuchunguza tukio la kuporomoka kwa Beit Al Ajaib ilki kupata ripoti ambayo itayosaidia kuwepo mpango muziri wa uhifadh wa Mji Mkongwe.

Tume itaangalia urasimu unaosababisha kutokea maafa, matumizi ya fedha ya tasisi hizo, utoaji wa vibali na muundo wa bodi ndani ya tasisi zilizopewa mamlaka ya kuungalia mji huo.

“Ninachotarajia katika tume ni pamoja na kuangalia sababu zilizopekea kuanguka kwa jengo na kutoa ushauri nini kifanyike ili kuweza kuendelea kuuhifadhi mji huo’’, aliongeza.

Taasisi zinazohusika na Mji Mkongwe ni pamoja na Mamlaka ya Mji Mkongwe, Shirika la Nyumba Zanzibar, Tasisi ya Wakfu na Mali ya Amana, nyumba za watu binafsi na tasisi za serikali.

Dk. Mwinyi alitaka majengo ambayo si salama kwa makazi yafungwe mara moja kabla ya kusababisha ajali.

Rais aliipongeza serikali ya Oman kwa kukubali kusaidia na kuwakaribisha wadau wengine kusaidia  iwe kwa fedha, kiutaalam au ushauri katika kuuhifadhi mji huo.

Aliahidi kwamba serikali itakuwa wa kwanza kutoa fedha za ukarabati wa Mji Mkongwe na kuona mji huo sio sehemu ya kutoa fedha na kuingiza pekee bali pia kuipatia  fedha serikali.

Alisema wadau wa utalii wamemuamabia kuwa tuna rasilimali kubwa, lakini zipo  ambazo hatuzitumii vizuri na hizi ni pamoja na Mji Mkongwe na hazijafanyika juhudi za kutosha za za kuutunza  kwa vizazi vya sasa na baadae.

Unapotaja historia ya Zanzibar, huwezi kuacha  kugusia mambo Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Visiwa hivi vina vitu ambavyo huwezi kuvipata katika nchi nyingi duniani.

Ili kuenzi utajiri huo watu wa Zanzibar hawana budi kutafuta njia sahihi za kuvihifadhi na kuvitunza kwa maslahi ya taifa na vizazi vijavyo.

Miongoni mwa majengo ya ni pamoja na jengo la Beit Al Ajaib ambalo historia yake sio kwa Zanzibar tu bali Tanzania, Afrika na dunia kwa ujumla.

 Beit el Ajaib iilijengwa kwa  udongo na chokaa na kusimamishwa na nguzo za chuma 48, ngazi kuu mbili na milango mikubwa 13.

Upande wa mbele wa jengo ulikuwepo mnara mkubwa ambao umeanguka na ulitumika kama kuwaongoza wanaosafiri kwa kutumia bahari.

Beit Al Ajab liliitwa ‘Jumba la ajabu’ kutokana na upekee wa jengo hilo katika Afrika Mashariki kutokana na kuwa jumba la kwanza kuwa na umeme, maji ya mfereji,lifti na miundombinu mengine katika ukanda huo. 

Ubunifu wa jumba hili ulifanywa na askari wa kikosi cha wanamaji kutoka Scotland na lilijengwa na Sultan Barghash bin Said mwaka wa 1883 ili kutumika kama  ofisi yake.

Matumizi ya jumba hilo yamekuwa yakibadilika na kati ya mwaka 1870-1888 (miaka 120 nyuma) ilikuwa ni kwa ajili ya sherehe za kitaifa za koo za masultani.

Hadi kufikia mwaka 1913 Waingereza walilifanya jumba hilo kuwa ofisi ya Serikali za Mitaa. Ofisi hizo zilidumu hadi wakati wa uhuru Disemba 10, 1963 na baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 jumba hilo lilitumika kama kumbukumbu za kilichokuwa chama cha Afro Shirazi Party (ASP) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Happo pia zilikuwepo gari alizotmia Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Jengo hili limekuwa linatumika kama kivutio cha utalii na ndani vikiwemo vitu  vya thamani na kumbukumbu za kihistoria.

Vitu hivyo ni kama vyombo walivyoitumia masultani, vitanda, mavazi, majambia, silaha, sehemu za kufanyia ibada na kumbi za mikutano.

Historia ya Zanzibar pia ni kielelezo cha utamaduni wa Wazanzibari wa kale na kukua kwa lugha ya Kiswahili.

Karibu miaka mitano iliopita sehemu ya jengo hili liliangukja na Serikali ya Oman ilisaidia kulitengenza na kubakia katika uhalisia wake.

Lakini wakati likitengenezwa mnamo Disemba 25 majira ya asubuhi upande wa kulia ulianguka na kusababisha hayo maafa.