NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya soka ya Small Rangers imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 4-0, dhidi ya vijana Kianga United ikiwa ni muendelezo wa mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo uliotimua vumbi majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Dole wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja.

Mabao ya Small Ranger yaliwekwa wavuni na Ally Iddi dakika ya 14 na bao la pili liliongezwa na Omar Said dakika ya 34, mabao yaliodumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.

Kurudi kipindi cha pili timu ya Small Rangers iliongeza mabao mawili ambapo bao la tatu lilifungwa na Ally dakika ya 67 na  bao la nne lilimaliziwa na Khalid Said dakika ya 78.