TOKYO,JAPANI

WAZIRI Mkuu wa Japani Suga Yoshihide amesisitizia dhamira yake ya kudhibiti ueneaji wa virusi vya korona na kuimarisha uchumi katika hotuba yake ya Mwaka mpya.

Suga alisema atafanya kila awezalo kuzuia ueneaji zaidi wa maambukizi na kulinda watu nchini Japani.

Aliongeza kuwa serikali yake itaunga mkono uwezekezaji utakaoleta uvumbuzi, na kuhamasisha mabadiliko katika sekta za kilimo na utalii ili kukuza chumi za maeneo.

Kuhusu sera ya mambo ya nje, Suga aliahidi kuwa atatafuta uhuru na uwazi wa eneo la Indo-Pasifiki, akitumia msingi wa ushirikiano kati ya Japani na Marekani.

Suga aliahidi kuwa serikali yake itaendelea na maandalizi ya kufanya Mashindano ya Olimpiki na Paralimpiki yaliyo salama katika msimu wa joto wa mwaka huu,yatakayoashiria  mshikamano wa ulimwengu.

Mashindano hayo ya Tokyo 2020 yalisogezwa mbele kwa mwaka mmoja kufuatia janga la virusi vya korona.