NA MWANDISHI WETU
CHAMA cha ADA Tadea kimesema ikiwa kweli Zanzibar imepania kujiletea maendeleo na kujijenga kiuchumi bila kuondoa muhali ,urasimu na kuhimiza nidhamu kwa watumishi wa umma mabadiliko yatakawia kupatikana.
Ushauri huo umetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa ADA TADEA, Rashid Yusuf Mchenga, wakati akizungumza na Zanzibar Leo Mjini Unguja, ambapo alisema wananchi wakiachwa kuishi kwa kutotambua thamani ya kazi na kukwamishana wenyewe kwa wenyewe mabadiliko yatakawia.
Alisema bila nidhamu katika kufanya kazi, kutolipaji kodi kwa nidhamu, matumizi ya fedha bila nidhamu na kutoetonda haki na wajibu Zanzibar itabaki kuchechemea wakati mataifa mengine duniani wanakimbilia maendeleo.
Mchenga alisema Mataifa yote duniani yaliopata maendeleo kwa haraka na kujijenga kiuchumi yamefanikiwa baada ya kukubali kujiendesha kwa misingi ya nidhamu ya kazi ,kujali uzalendo na wananchi wake kupendana bila kukwamisha wenyewe kwa wenyewa.
Alisema Zanzibar chini ya utawala wa awamu ya nane unaoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, bila kutiliwa mkazo masuala hayo , nchi haitafika mahali inapotarajia na ni vyema jamii ikabadilika kumsaidia Rais aliyepo madarakani.
“Ikiwa nchi itaongozwa kwa kuhimiza nidhamu ya kazi. Watumishi ,wafanyakazi na watendaji katika ngazi wakiwajibika kwa nidhamu. Wafanyabiashara, wakulima, wavuvi na wafanyakazi watakapotilia maanani nidhamu hapo ndipo maendeleo yayakapoonekana “Alisema Mchenga.
Alisema Zanzibar haina sababu ya kukwama kimaendeleo na wananchi wake kukosa maisha bora na yenye neema kwakuwa suala la nidhamu linekuwa likipuuzwa huku mambo yamsingi yakikendeshwa “kiswahili”.
“Tumebahatika kuwa na tunu za amani, umoja na utulivu kwa miaka mingi .Tumefika mahali tulipo kwakuwa tu masuala ya uwajibikaji, upendeleo na ubaguzi .Haiwezekani mtu asiye na weledi, hana ubunifu wala maarifa ya kutosha kitaaluma apewe dhamana ya utendaji “Alieleza.