NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Chama cha Taekwondo Mkoa wa Dar es Salaam (DTA) umeandaa semina maalum kwa wanawake .

Akizungumza kwenye semina ya wakufunzi wa mchezo huo iliyofanyika Ijumaa, Mkurugenzi wa Ufundi wa DTA Majaliwa Patrick, alisema walengwa na semina ni wale wasiofahamu mchezo huo .

Patrick alisema lengo ni kuwafundisha kwa kuwaelezea faida zake ,ushiriki katika mashindano mbalimbali ili kuwaondoa katika mtazamo hasi kwa wanawake.

Alisema washiriki hao watatoka vyuoni, skuli mbalimbali kwa nia ya kuhamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchezo huo.

Naye Katibu Mkuu wa DTA Erasto Golyama, alisema wakufunzi hao wanatakiwa kwenda kufanya kwa vitendo yale waliojifunza katika maeneo yao.

Alisema watakuwa na jukumu la kuwaandaa wanafunzi, wachezaji mbalimbali kutoka klabu mbakimbali.

Wakufunzi 23 wamefaidika na semina hiyo ambayo ilifanyika kwa siku moja jijini Dar es Salaam.