NA JOSEPH NGILISHO ARUSHA
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Arusha (TAKUKURU) inachunguza kiasi Cha sh, Milioni, 933,866,399.68 Ilizokopwa na SACCOS za mashirika makubwa ya umma Mkoa wa Arusha AICC SACCOS na AUWSA SACOOS kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii PSSF na kushindwa kurejesha kwa wakati
Akiongea na waandishi wa hàbari wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya utendaji kazi ofisini kwake , Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, James Ruge alifafanua kwamba katika kiasi hicho SACCOS ya kituo Cha kimataifa cha mikutano AICC SACCOS ilikopa kiasi Cha sh,milioni 435,754,794.46 na kushindwa kulipa kwa wakati
Aidha Saccos ya Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira mkoa wa Arusha AUWSA ilikopa kiasi Cha sh, milioni 498,111,609.47 na kushindwa kurejesha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano na hivyo takukuru umeanza uchinguzi was kuzirejesha kwa mujibu wa Sheria.
Aliongeza kuwa taasisi hiyo pia ipo katika hatua ya kurejesha kiasi Cha shilingi milioni 414,901,264 zilizotokana na mkopo wa Matrekta uliotolewa na Mfuko wa Pembejeo wa wizara ya Kilimo kwa wakulima kumi wa halmashauri ya Meru, Arusha na Monduli Kati ya mwaka 2013 hadi 2016 .
Alisema fedha hizo zilitolewa na shirika la maendeleo la Taifa NDC kwa lengo la kuwasaidia wakulima kuondokana na umasikini wa kutumia jembe la mkono .
Amewataka wakulima wote wa mkoa wa Arusha waliopata mkopo wa madrekta kupuuza upotoshaji unaoenezwa kwamba mkopo wa serikali kuwa hairejeshwi.
Katika hatua nyingine Ruge amesema kwamba katika kipindi Cha miezi mitatu ya Oktoba,Novemba na Disemba Takukuru Mkoani hapa imefanikiwa kurejesha fedha na Mali zenye thamani ya sh,milioni 578,580,334 .
Alisema kati ya fedha hizo sh,milioni 365,580,334 ni fedha thaslimu.
Alisema fedha hizo ni Kodi ya serikali ,Madeni ya vyama vya ushirika na Madi binafsi ya wananchi wanyonge yaliyokuwa kwenye hatari ya kupotea kutokana na ubadhilifu ,shuluma na utapeli.